}

TALGWU YAISHUKURU SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI WATUMISHI WALIOONDOLEWA KWAKUKOSA SIFA ELIMU YA KIDATO CHA NNE.

Na.Happy Shirima.
Chama Cha wafanyakazi wa serekali za mitaa Tanzania (TALGWU) kimeishukuru serekali kwa kuzingatia mapendekezo yaliyowasilishwa na chama hicho na kuamua kuwarudisha kazini watumishi waliondolewa kwa kukosa sifa za kuwa na elimu ya kidato Cha nne.

Akizungumza jijini Dar es salaam katibu wa chama hicho Rashid Mtima amesemakuwa  pamoja na watumishi hao kurejeshwa kazini pia watalipwa mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria.

Aidha ameongeza kuwa katika utekelezaji wa agizo La kuwaondoa watumishi hao kwenye mfumo wa malipo baadhi ya waajiri katika halmashauri mbalimbali walifanya tafsiri potofu ya kuwaondoa pamoja na watumishi wenye elimu ya darasa la Saba walioajiriwa kabla ya Mei  2004 licha ya agizo hilo  kuwahusu walioajiriwa kuanzia Mei 20 mwaka 2004 na kuendelea.


Hata hivyo agizo hilo lilipelekea jumla ya wanachama 7,382 kuondolewa kazini na chama kupoteza wanachama zaidi elfu tatu wakiwemo watendaji wa kata , vijiji na mitaa wapatao 2,098 pamoja na kada nyingine.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Aprili 9 mwaka huu waziri wa nchi ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi was umma na utawala bora kapteni mstaafu George Mkuchika kutoa kauli ya serekali  bungeni ya kuwarejesha watumishi hao kazini mara moja pamoja na kulipwa mishahara yao.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.