}

MADAKTARI BINGWA KUTOKA MOI WAANZA UPASUAJI WATOTO WENYE MATATIZO YA VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI NACHINGWEA.

Na.Geofrey Jacka-Lindi.
Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), wameanza upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Zoezi hilo limepangwa kudumu kwa siku tatu kuanzia Tarehe 14 April 2018 hadi Jumatatu ya tarehe 16 April 2018 ambapo pia itafanyika clinic kwa walioshindwa kufika MOI siku za nyuma.
Akizungumzia zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh.Rukia Muwango amesema, katika Zoezi hilo watoto 15 watafanyiwa upasuaji, na wengine watapata ushauri wa Kitabibu, huku akijivunia kusababisha upatikanaji wa huduma iyo muhimu kwa watoto wa Nachingwea Mkoa wa Lindi na mikoa ya jirani, hususan Mtwara na Ruvuma.

"Kwakweli najivunia sana kuileta huduma hii, pia natoa shukrani  zangu  za dhati kabisa kwa Uongozi wa MOI kwa kukubali ombi langu na kunipa ushirikiano tangu mwanzo wa kampeni hii hadi sasa tunavyohitimisha zoezi hili kwa kukamilisha matibabu". Alisema Muwango.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.