}

TAIFA STARS KUWAKABILI ALJERIA MARCHI 22, SERENGETI BOYS YAENDELEA NA MAZOEZI KUISUBILI CECAFA


Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.
Stars itasafiri kuelekea jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria Machi 22, 2018 na baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Pia Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys inaendelea kujiandaa na mashindano ya CECAFA kwa vijana yatakayofanyika Burundi.
Kikosi hicho kipo kambini kwenye hostel za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF,Karume-Ilala,Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya CECAFA kwa Vijana yataanza April 1 mpaka April 15 huko Burundi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.