}

REPOA YATOA UTAFITI WA MWENENDO WA UCHUMI WA NCHI NA HALI ZA MAISHA ZA WATANZANIA.

Na. Happy Shirima-Dar.
Mkurugenzi mtendaji wa Repoa Dk.Dornald Mmari.
Taasisi isiyokuwa ya kiserekali inayojishughulisha na utafiti, masuala ya uchumi, umaskini na maendeleo ya nchi Repoa imewasilisha matokeo ya utafiti unaohusu maoni ya wananchi juu ya hali ya uendeshaji wa uchumi wa nchi pamoja na hali zao za maisha.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo uliopewa jina la AFRO BAROMETER kwa mwaka 2014 / 2017 Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dkt Dornald Mmari amesema kuwa matokeo yanaonesha kuwa wananchi wanamatumaini na jinsi ambavyo uchumi unaendeshwa na kuamini kuwa hali yao ya maisha ndani ya kipindi kifupi itabadilika.

Aidha utafiti huo umeonesha baadhi ya maeneo ambayo yameonekana kuwa na changamoto  ni eneo la ajira, ambapo Kwa mwaka 2014 ilikuwa asilimia 54 na kwa mwaka 2017 umeshuka hadi asilimia 31 huku uhakika wa mlo kwa mwaka 2014 ulikuwa asilimia 43 ambapo mwaka 2017 umeshuka hadi asilimia 23. 

Amesema katika utafiti wao wamebaini kuwa changamoto hizo zinatokana na mfumo wa kiuchumi ambao unategemea sekta ambazo azijengi ajira za kipato kama kilimo kidogo.

"Kinachotakiwa ni kubadilika kwa taswira ya uchumi na ndio mana Serikali ya awamu ya tano imeweka mkazo katika uchumi wa viwanda ili kutengeneza ajira ambazo ni za uhakika", amesema Mmari.

Kwa upande wake Mtafiti wa Repoa Steven Mombera amesema kuwa utafiti huo umefanyika katika maeneo yote ya Tanzania bara na Zanzibar huku ukizingatia idadi ya watu kutokana na takwimu za sensa ya watu na makazi za ofisini ya taifa ya Takwimu (NBS) kwenye mikoa yote ambapo wamefanikiwa kuhoji  watu 2400.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.