}

OKWII KAMA KAWA KIKOSINI KESHO DHIDI YA STAND UNITED


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa 19 inaendelea kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya  Shinyanga
Mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Mshambuliaji wa tishio wa klabu hiyo ya simba Emanuel Okwi ameendelea na mazoezi leo kwa ajili ya mchezo huo 

meneja wa klabu ya simba Richard Robert amesema kikosi chote kipo katika mazoezi isipokuwa mchezaji Haruna Niyonzima ambaye ndiye majeruhi pekee atakaekosekana katika mchezo wa kesho.

Robert  pia amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri na wanaamni kesho watafanya kile ambacho mashabiki wa klabu hiyo wanakihitaji.

'tunaihesimu sana stand united lakini hatuna sababu ya kupoteza katika mchezo huo, tunaamini itakuwa ngumu kupata matokeo ila inabaki kazi ya wachezaji kufanikisha kile ambacho tumekitoa kwao.' alisema  Robert.

katika mchezo huo hapo kesho tff imewatangaza waamuzi watakaochezesha mchezo huo.

Mwamuzi wa katikati Florentina Zabron kutokea Dodoma ,Mwamuzi msaidizi namba moja Ferdinand Chacha wa Mwanza,mwamuzi msaidizi namba mbili Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza,mwamuzi wa akiba Gelmina Simon wa Dar es Salaam na kamishna wa mechi anatoka Arusha,Peter Temu.
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.