}

MBONDE NA NDUDA KUREJEA KIKOSINI WIKI IJAYO



Kipa namba mbili wa Simba, Said Mohammed 'Nduda' wiki ijayo anatarajia kujiunga na wenzake tayari kuanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa miezi mitano, kufuatia kufanyiwa upasuaji wa goti Oktoba mwaka jana nchini India.

Nduda alianza mazoezi yake binafsi tangu mwanzoji mwa mwaka huu, akijifua ufukweni na gym. 


 Nduda aliyesajiliwa Simba Julai mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, hajacheza mechi yoyote msimu huu kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata Agosti mwaka jana mazoezini 
 kambini visiwani Zanzibar wakati Simba inajiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga Agosti 23, mwaka jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Beki wa kati wa Simba, Salim Mbonde anaendelea na mazoezi ya gym baada ya kuwa nje kwa  zaidi ya miezi mitatu kufuatia kuumia Oktoba 15, mwaka jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar uliomalizika kwa sare ya 1-1 mjini Dar es Salaam.

Mbonde aliye katika msimu wake wa kwanza pia Simba tangu aondoke Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar anatarajia kuanza mazoezi wiki ijayo.



No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.