}

KIFAA CHA KUJIPIMA SARATANI UKIWA NYUMBANI CHAZINDULIWA DAR KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI.

Na. Happy Shirima.

Katika kuadhimisha siku ya saratani duniani hospitali ya Agakhani kwa kushirikiana na hospitali ya taifa Muhimbili na Life line pharmacy wamezindua kampeni ya upimaji wa awali wa saratani ya utumbo mpana pamoja na kipimo cha colorectal Cancer ambacho mtu anaweza kujipima  akiwa nyumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kitengo cha saratani na Daktari bingwa wa ugonjwa huo kutoka hospitali ya Agakhani Harson Chuwa amesemakuwa idadi ya wagonjwa wa saratani imekuwa ikiongezeka kila siku ikiwa ni pamoja na ile ya utumbo mpana ambayo imekuwa haitiliwi mkazo.
Aidha Dr.Chuwa ameongeza kuwa  kampeni hiyo itakuwa endelevu ambapo wananchi watafanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya utumbo mpana pamoja na kupewa elimu ya jinsi ya kujikinga na saratani ambapo pia kutakuwepo na kipimo cha colorectal Cancer ambacho kitawasaidia wale ambao wanashindwa kufika hospitali kujipima wakiwa nyumbani.

Kwa upande wake Afisa uhamasishaji damu salama kanda ya mashariki             Fatuma Mjungu amesemakuwa ongezeko la ugonjwa wa saratani linaendana na uhitaji wa damu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa saratani imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha damu kuliko magonjwa menginie ambapo asilimia 25 ya damu inayokusanywa inatumiwa na wagonjwa saratani wakifuatiwa na watoto na kinamama.

Hata hivyo dalili za ugonjwa wa saratani ya utumbo mpana ni pamoja na maumivu kwenye utumbo, choo kuwa chembamba na kuchanganyika na damu ambapo asilimia 95 ya wagonjwa wanaowahi mapema hospitali hutibiwa na  kupona.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.