COULTINHO ; NAIPENDA LIVERPOOL KUTOKA MOYONI
Kiungo mshambuliaji wa Brazil na timu ya barcelona kwa sasa Phillipe Coultinho amesema hataisahau klabu yake ya zamani ya liverpool baada ya kuelekea kunako klabu ya Barcelona
Coultinho Juzi amekamilisha kandarasi yake ya kuitumikia klabu ya barcelona akitokea liverpool amethibitisha kuelekea huko barca ni ndoto yake ya muda mrefu
Amesema Tangu alipowasili kunako kikosi cha Liverpool yeye na familia yake amejisikia faraja juu ya mapokezi yake na alipata marafiki wengi katika klabu hiyo
Ndani ya uwanja na nje nimepata uzoefu mzuri wa klabu pamoja na mashabiki wake na kunirejeshea kumbukumbu na nyakati ambazo zimenipa furaha kutoka kwa mashabiki wa klabu ya liverpool,alisema.
No comments