}

BOCCO RASMI UNAHODHA MSIMBAZI

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba SC, Mrundi Masud Juma Irambona leo amemthibitisha mshambuliaji mzoefu, John Raphael Bocco kuwa Nahodha mpya wa timu hiyo, kufuatia kuondoka kwa beki Mzimbabwe, Method Mwanjali.

Taarifa ya Simba SC iliyotolewa na Mkuu wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hajji Sunday Manara imesema kwamba Bocco atakuwa anasaidiwa na beki wa pembeni, Mohammed Hussein 'Tshabalala' pamoja na kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto. 


“Uthibitisho huo umeungwa mkono na uongozi wa klabu na unaamini utaongeza ari zaidi ndani ya timu, sambamba na nidhamu kwenye kikosi chetu,”imesema taarifa ya Manara.


Na uteuzi huo unafanyika katika siku ambayo Simba 
itamenyana na timu ya zamani ya Bocco, Azam FC usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.