}

TANROADS YASAINI TZS.BILIONI 362 UJENZI WA BARABARA.

Serikali kupitia wakala wa barabara Nchini Tanroads imesiani mikataba minne ya miradi ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 404.979 zitakazogharimu zaidi ya sh. Biloni 362.

Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo jjini Dar es salaam waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara ya Tabora(usesula) koga hadi mpanda yenye urefu wa km 335 na mbinga hadi mbamba bay yenye urefu wa km 67.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Tanroads Mhandisi Patric Mfugale amesema fedha za mradi huo zimetoka katika benki ya maendeleo ya afrika na mfuko wa maendeleo Afrika ambapo mradi wote unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi 36.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.