}

ACCOUNT YA MANGE KIMAMBI YAFUTWA RASMI INSTAGRAM.


Uongozi wa mtandao wa Instagram umeamua kuiondoa/kuifuta account ya Mwanadada Mange Kimambi iliyokuwa na followers milioni moja na laki tano katika matumizi kwa kuonekana kuvunja taratibu na miiko ama masharti ya Instagram. 

Imeonekana kuna watu wamekuwa waki ripoti juu ya aidha taarifa za Mange kama zisizoendana ama kuvunja maadili kitu kilichopelekea kufutwa kwa akaunti hiyo.

Uongozi huo umesema katika taarifa hiyo ya kuundoa ukurasa huo. " Tumeufuta ukurasa wa Mange Kimabi. Tunashukuru kwa taarifa juu ya account hii. Tumeuondoa ukurasa huu kwa sababu ya kukiuka masharti. Taarifa yako ni muhimu sana ili kuitoikosea jamii kwa mambo yasiyofaa".
 
Inaonekana taarifa imekuwa ni kwa wingi sana kuuripoti ukurasa huu, lakini taarifa nyingine zinasema kuwa Mange ameamua kuachana na mitandao ya kijamii hususan Instagram huku watu wake wa karibu wamenukuliwa wakisema kuwa Mange amechoka kuwapigania haki Watanzania kwa kuwa wenyewe hawako tayari.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.