}

WATAALAMU WA TEHAMA FANYENI KAZI KWA WELEDI-NAIBU WAZIRI MAWASILIANO.

Na. Happy Shirima-Dar.


Naibu waziri uchukuzi na mawasiliano mhandisi Atashasta Nditiye amewataka wataalamu wa  teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia miiko yao ya kazi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mhandisi Nditiye amesemakuwa  taaluma ya tehama imekuwa ikichangia pato la taifa pamoja na kutengeneza ajira kwa wananchi hivyo  mtu yeyote atakaechafua taaluma hiyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha amelitaka baraza la watumiaji huduma za mawasiliano nchini kukutana na watoa huduma za mawasiliano ili kujua sababu za kutoonekana kwa baadhi ya chaneli za TV 5 za Tanzania ambazo zilikuwa zitnatolewa bure.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa tume ya taifa ya TEHAMA Mhandisi Samson Mwela amesemakuwa wataalamu wa TEHAMA wanatakiwa kusajiliwa kushirikishwa na kutambulika ili kuongeza uzalishaji ambapo utafiti umeonyesha kuwa kati ya bidhaa laki moja zinazozalishwa hapa nchini bidhaa 4 tu ndio za TEHAMA

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.