}

NENO LA ABDUL MKEYENGE SHABIKI WA CHELSEA

ABDUL MKEYENGE
WHAT a cross. What a header. Ni maneno yaliyotoka vinywani mwa Peter Drury na Jim Belgin waliokuwa watangazaji. Hapo walikuwa wakilisherehesha bao la Morata aliyeunganisha krosi ya Azzipicuelta kwa kupiga kichwa kilichokwenda hewani kama ndege ya Bombardier ikikata mawimbi ya jua.
Asikwambie mtu, kwangu hakuna ushindi mzuri wa Chelsea kama kuifunga Manchester United, sijui kwa mashabiki wenzangu wao wanajisikia furaha tukiifunga timu ipi. Uzuri zaidi naupenda ukimya wao ukiwafunga. Huu ukimya ulioko sasa ni moja ya kitu ninachokipenda kutoka kwao.
United wakifungwa wanakuwa na nidhamu na wanyenyekevu. Naiona nidhamu yao ya juu kabisa kutoka jana mpaka leo mitandaoni na nje ya mitandao. Naipenda sana hali hii. Alafu kama wameambiana vile kwa pamoja kuwa wazime data, ili wasitoe ushirikiano. Ushabiki gani huu jamani? Njoeni tuzungumze ball. Acheni rikaka.
Siku nyingi sikuja na vitu vya namna hii, na wao United ndiyo waliokuwa wakiniulizia yuwapi Mkeyenge leo nimekuja kwa ajili yao nimekimbiwa. Ina maana 'mliya'mis' maandiko ghafla mkayachukia? Ziko wapi zile jeuri zenu? Njoeni basi. Inakuwaje tutazame mpira pamoja, lakini kwenye maandiko nabaki mwenyewe? Njoeni! Basi Siwatanii tena.
Kukereka kwenu na matokeo ya jana na kukereka kwenu na maandiko ya namna hii mpaka mnazima data bila sababu, hayo ndiyo maisha mliyojichagulia kuishi. Hivi mnadhani kununa kwenu, ndiyo dawa? Dawa ni kuhana hapo mlipo na kujiunga Chelsea. Hakuna dawa nyingine ya kuepeuka maneno haya. La sivyo yatakuwepo kila siku.
Ningekuwa mchoyo kama asubuhi hii ya Blue Monday nisingekuja na andiko hili. Hili ni andiko linalopaswa kuja muda huu kuwakumbusha watu kuwa sisi ni Chelsea na wanadamu wa aina ya Mkeyenge ndiyo mashabiki wake. Wengi mlisahau hili na mwisho mkawa mnalopoka kama mmekunywa maji ya chooni. Leo nimeamua kuwakumbusha kuwa Chelsea ipo na Mkeyenge nipo pia.
Wakati mwingine ukimuona kobe kainama sio kama anakuwa amekufa, mainamio yake yanajikita kwenye utungaji wa sheria. Kiwango cha Chelsea mwanzoni mwa msimu kiliwatoa watu mapovu, aibu iliyoje wale wote waliomwaga povu leo wako kimya na wamezima data. Ila niwaambie mlichokifanya sio uungwana. Njoeni tuzodoane, tusemane, tupigane masingi. Mpira ndiyo ulivyo.
Muda mwingi ambao United walitamba humu mitandaoni kwa kushinda vile vibao vyao vinne vinne na kuzifunga timu dhaifu za nafasi ya 11 kwenda 20, na sio kuzifunga timu za nafasi ya 10 kushuka 1, nilitamani ije mechi ya namna hii. Niliitamani sana na nilitamani hii hali. Wote kimyaaaaaaaaaaaa.
Walivyokuja Stamford Bridge jana kuna vitu walivisahau Old Trafford. Walimsahau Herrera. Hivi jana alikuwepo uwanjani? Mbona Hazard katembea sana na kacheza kadri anavyojisikia? Nilitaraji uwepo wa Herrera kupunguza movement za Hazard. Next time mkija Stamford Bridge njoeni nae. Jana tulim'mic.
Morata na Lukaku! Sasa tumepata majibu. Morata ni mchezaji wa timu kubwa mwenye kufunga mechi kubwa. Lukaku ni mchezaji wa timu ndogo anayezifunga timu ndogo na wapuuzi wenzake ndiyo wanaomshangilia. Hizo ndiyo tofauti zao. Mapovu ruksaaaaaaaaa, matusi no. Sasa jifanye unajua kutukana.
Ukileta tusi nina wewe. Tena muda huu ninaokaribia kuoa ukinitukana tu korokoroni kunakuhusu ukanilipe faini ili niongeze fedha za vitambaa vya blue kama rangi ya Chelsea ambavyo nataka viupambe uwanja wa siku yangu ya ndoa. Mkija njoeni kwa hoja. Sitanii jamani. Narudia tena, matusi no. No. No. No. No. No. No. No. No. No. No. No. No. No. No. No.
Kama ukiona nazidi kukukera na maneno haya unaweza kuni'unfriend. Fanya hivyo ili uwe salama, vingine na hapo kila siku inakuja moja kama hii, ukiamka asubuhi unaiona mbele ya simu yako. Hili ni zoezi litakalodumu ndani ya wiki nzima. Haishii leo. Nitaendelea kuandika makala za namna hii mfululizo. Na kesho tena. Jiandaeni kisaikolojia.
Anyway ndiyo nimeamka hapa kitandani, lakini kama najiona vile leo nikiwa ofisini. Kuna watu wakiniona watanuna na watavaa earphone muda mrefu ili kulikwepa domo hili, lakini niwaambie wasijisimbue kufanya hivyo, hii dozi itakuwa ya wiki nzima. Itakuwepo leo, itakuwepo kesho, itakuwepo keshokutwa, itakuwepo mtindo goo. Mpaka wiki iishe. Nina nyinyi wiki hii, mpaka mseme poo.
Katika paragraph hii ya mwisho nitakuwa si mkarimu kwa wageni nikiishia kuandika maneno mengi yaliyowakera na kuwachoma kisha nikaacha kuwaambia asanteni kwa kuja ( Thanks for coming). Poleni sana kwa kila kilichowatokea, rudini mkajipange kisha tuonane wakati mwingine mkiwa na Herrera.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.