}

NDIKUMANA AFARIKI SIKU CHACHE BAADA YA NDOA YA UWOYA NA DOGO JANJA.

Hamad Ndikumana akiwa na mkewe na muigizaji maarufu nchini Tanzania Irene uwoya.
Habari ya kusikitisha, mume wa zamani za Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia.

Alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda. Uongozi wa timu hiyo umesema jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya. 

Mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajapata ajali. 

Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake kwani miili ya waislamu haihifadhiwi katika monchwari za kawaida kwa mujibu wa imani zao. 

Hamad Ndikumana alijulikana kama Kataut kwamujibu wa mashabiki wa soka wa nchini Rwanda, alizaliwa Oktoba 05/1978 mjini Kigali Rwanda, alikuwa na urefu wa futi 5 na inchi 11.

Mara ya mwisho Kataut aliichezea timu ya Stand United ya mjini Singida hapa Nchini Tanzania.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.