MH.MAKONDA; NITAHAKIKISHA UGONJWA WA AHMED ULIOMTESA KWA MIAKA 10 UNAMALIZIKA.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda(Mwenye koti jeusi) akizungumza jambo na kijana Ahmed aliyedumu na ugonjwa kwa miaka kumi. |
AHMED ALBAITY anatakiwa kwenda kutibiwa Nchini China kwa muda wa Wiki tatu akiambatana na Wasaidizi Wawili ambapo Gharama za Matibabu zinazohitajika ni zaidi ya Dola 40,000 za Marekani ambapo Sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha Dolla 27,000.
RC MAKONDA amesema atafanya jitihada zote kuhakikisha AHMED anapatiwa Matibiwa ili aweze kupona na kutimiza ndoto zake akiwa na Afya Njema.
No comments