}

MBEYA CITY IKO KAMILI KUWAVAA MBAO CCM KIRUMBA KESHO




Ligi Kuu Tanzania bara raundi ya 6 inaendelea tena wiki hii katika viwanja mbalimbali nchini na mchezo nambari 41 utazikutanisha MBEYA CITY  na Mbao FC ya jijini Mwanza. Mchezo huu utakaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba  na utahitimisha mechi tatu za mwanzo za ugenini baada ya mchezo dhidi ya  Stand na Mwadui katika kanda ya ziwa.

Mbeya City FC inaingia katika mchezo huu ikiwa na rekodi ya kuifunga timu hiyo mpya katika ligi ya Tanzania bara nyumbani na ugenini. Msimu uliopita mchezo wa kwanza uliochezwa CCM Kirumba Mbeya City FC iliibuka na ushindi wa magoli 4 kwa 1, magoli hayo yakifungwa na Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Rafael Daud Ambaye kwa sasa anakitumikia kikosi cha yanga na Omary Ramadhani. 

Duru la pili katika uwanja wa Sokoine kwa mara nyingine tena Mbeya City iliibuka na ushindi mwingine wa magoli 3-1, magoli yaliyowekwa wavuni na Zahoro Pazzi, Tito Okelo na Rafael Daud.

Rekodi hii ya magoli 7 kwa 2 dhidi ya mbao inaiweka klabu ya mbeya city katika nafasi kubwa zaidi ya kushinda mechi hii itakayochezwa hapo kesho  majira ya saa kumi jioni; 

Meneja wa Timu Geofrey Katepa amezungumza na  kuelekea mchezo huo hapo kesho  ambapo amesema wamewasili  salama jijini Mwanza, hali ya hewa imepoa na hakuna joto sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. 

Katepa amesema  wanaamini mchezo huo utakuwa  mzuri  maana kikosi chao chote kiko ‘fiti’ na hakuna majeruhi kabisa’.

Kocha Ramadhani anakwenda kuongoza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi cha dhambarau kutoka Jijini Mbeya na hii itakua mechi yake ya kumbukumbu katika soka la Tanzania.

Mchezo utakaofuata baada ya huu wa Mbao FC utachezwa katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya dhidi ya Ruvu Shooting tarehe 21.10.17.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.