}

TUKIREJEA KILELENI LEO HATUSHUKI TENA

SIMBA SC itakuwa na kibarua kizito cha kuhakikisha inarejea kileleni mwa ligi kuu  Tanzania Bara wakati itakapomenyana na Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog itaingia kwenye mchezo wa leo akiwa na lengo
moja tu la kuhakikisha anapata ushindi ambao utamrejesha katika kileleni cha Ligi Kuu.

Endapo simba watafanikiwa kupata ushindi hii leo basi watarejea kilele kutokana kwa sababu wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Yanga SC hawatakuwa na mechi ya Ligi Kuu wikiendi hii kwa kuwa wamekwenda Comoro kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kikosi cha Yanga kimetua salama nchini Comoro ikiwa ni maandalizi ya mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga itacheza na wenyeji Ngaya ambao wanaelezwa kuwa wameimarika na soka la Comoro limekuwa likipanda.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema wako makini na hawatafanya mzaha.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.