}

Mbunge wa Ilemela akutana na vijana wa Ilemela wanaoichezea timu ya Taifa ya vijana Serengeti boys.

Na. Anaseli Stanley Macha.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula Leo amekutana na Vijana wa Ilemela wanaoichezea Timu ya   Mpira wa miguu ya Vijana nchini  Serengeti Boys

Timu ya Wavulana Serengeti Leo imefanya Ziara ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma

Akizungumza na Wageni hao Mbunge wa Ilemela amewahakikishia kuendeleza  ushirikiano katika kukuza Michezo ndani ya Jimbo na nje ya Jimbo  huku akiwapongeza kwa mafanikio na heshima waliyoiletea Taifa sambamba na kuwataka kuacha kubweteka na kuongeza juhudi ili kupata mafanikio zaidi ya waliyonayo sasa

Hivi karibuni Mbunge wa Ilemela mbali na kufanya kampeni ya kukuza Elimu ameendeleza kampeni ya kuhakikisha anakuza vipaji vya michezo mbalimbali jimboni kwake kwa kuanzisha Angeline Ilemela Jimbo Cup na Maazimisho ya kumkumbuka aliyekuwa mchezaji wa Mbao Fc Ismail Mrisho ikiwa ni mkakati wa kuifanya Michezo kuwa Ajira

Jumla ya wachezaji wapatao Wanne wanaotoka Jimbo la Ilemela wamepata fursa ya kuichezea Timu ya Vijana ya Taifa Serengeti wakiwemo Ally Hussein, Israel Patrick, Ally Hamis na Kelvin Nashon

Wakati huo huo Mhe Mabula ameendelea kuwawakilisha vema wananchi wa Jimbo la Ilemela jioni ya Leo katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.