}

Manji amjibu Paul Makonda, aapa kumfungulia Kesi mahakamani.

Na. Geofrey Donatus Jacka.

Yusuph Manji.
Yusuph Manji amekuwa miongoni mwa watu zaidi ya siti ambao majina yao yametajwa Leo hii na Mh. Paul Makonda mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wakituhumiwa kwa Uuzaji wa Madawa ya kulevya.

Muda mfupi baada ya Mh. Makonda kutaja majinina hayo naye Yusuph manji alijitokeza nakuwaita waandishi wa habari nakuzungumza mambo mazito ikiwemo kuonesha nia yakumfungulia kesi mahakamani kwakumdhalilisha huku akisisitiza kuwa hatosubiri siku ya Ijumaa kuonana na Makonda Bali atakwenda kuonana nae  kesho kwakuwa hatoweza kupanga foleni ya watu zaidi ya Sitini siku ya Ijumaa.

Akizungumza na waandishi Manji ameongeza kuwa vipo vifungu vya sheria katika katiba ambavyo vinamlinda hivyo haoni sababu yakutomfungulia mashtaka Mh. Makonda.

Paul Makonda aliyataja majina Leo hii ikiwa ni awamu ya pili ya vita yake aliyoianzisha dhidi ya Madawa ya kulevya hu akisisitiza kuwa kama atashindwa vita hii basi si yeye peke yake Bali itakuwa ni taifa zima ndio limeshindwa.
Mh. Paul Makonda. (Picha na Anaseli Stanley Macha) 


Zifuatazo ni picha zinazoonesha majina ya watu waliotajwa Leo hii na mheshimiwa Makonda akiwatuhumu katika biashara ya Madawa ya kulevya.




Watu wengi wanamfahamu Manji kupitia kujihusisha kwake katika michezo akiwa ni mmoja kati ya viongozi wa klabu ya mpira wa miguu ya Yanga lakini Manji ni mfanyabiashara mkubwa akiwa ni miongoni mwa Mabilionea wakubwa wanaotambulika ndani na nje ya nchi. 







No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.