}

Miili ya wachezaji wa Chapecoense ya Brazili yapokelewa kwa simanzi.


Watu wapatao Laki moja wamejitokeza katika uwanja wa Chapecoense huko kusini mwa Brazil ili kuipokea miili ya wachezaji waliofariki katika ajali ya ndege huko Colombia.

Licha ya Mvua kubwa kunyesha lakini watu walisubiri ili wapate nafasi ya kuipokea miili ya ndugu zao ili kuipa salamu za mwisho tayari kwa mazishi.

Chanzo cha ajali ya ndege iliyoua wachezaji hao bado hakijawekwa wazi lakini inasemekana rubani aliwasiliana na chumba chakuongoza ndege akiomba kutua kwakuwa ndege imeishiwa mafuta.

Ajali iliua watu 71 wakiwemo wa Brazil 64, watu wa jamhuri ya Bolivia 6, Venezuela na watu wa Paragwai.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.