}

Kamishna Jenerali wa Magereza asitisha mkataba wake wa kazi.

Na. Geofrey Donatus Jacka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli, amekubali na kuridhia Ombi la kusitisha Mkataba nakustaafu kwa mkuu wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Casmir Minja kuanzia Desemaba 2 .

Hii imekuja siku chache baada ya Rais kutembelea gereza la Ukonga la jijini Dar nakupata fursa yakuzungumza na Maafisa na Askari wa Gereza hill ambapo Rais Magufuli alitoa maagizo mbalimbali yahusuyo Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku askari kujinunulia sare za jeshi huku akisema kuwa hana taarifa kama jeshi hilo lina shida ya sare za kazini, lakini pia alitoa shilingi bilioni 10 zakujenga makazi ya Askari hao.

Rais Magufuli amempongeza Minja kwautumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu, wakati huohuo amemteua Kamishna wa Magereza Dk. Juma Malewa kukaimu nafasi hiyo.

Minja ni kiongozi wa 17 kuliongoza Jeshi la Magereza tangu lilipojitenga na Polisi na ni kiongozi wa 19 ukijumlisja kabla hawajajitenga na polisi.

Ikumbukwe kuwa kabla ya tarehe 25/08/1931 Utawala na Uongozi wa Jeshi la Magereza na Polisi ulikuwa Pamoja.

VIONGOZI WENGINE WALIOWAHI KULIONGOZA JESHI LA MAGEREZA NI KAMA IFUATAVYO:-

1.G. H -Heaton- 1931-1938
2.H. E Taylor -1938-1938
3.Milner -1938-1940
4. Dollan -1940-1943
5.W. A Browson -1943-1946
6.T. H Browson - 1946-1955
7.P. Manley 1955-1962
8.O. K Rugimbana 1962-1967
9.R. Nyamka 1967-1977
10.A. B Mwaijande 1978-1978
11. G. G Gineya 1979-1983
12.S. A Mwanguku 1983-1992
13. J. H Mangara 1992-1996
14. O. E Malisa 1996-2002
15. N. P Banzi 2002-2007
16. A. Nanyaro 2007-2012
17.John Minja. 2012-2016

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.