}

Hii hapa aina mpya ya Mkopo, imezinduliwa na FAIDIKA.

Na. Anaseli Stanley Macha.


Taasisi ya kibenki ya Faidika nchini, imezindua aina mpya ya mkopo ijulikanayo kama ‘Executive Loan’, ikiwa na lengo la kukuza utamaduni wa  matumizi ya huduma za kibenki nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. Mbuso Blamini, amesema mkopo huo mpya unaendana na lengo chapa la taasisi la ‘kuboresha Maisha’ ambao ni njia nyingine mpya kwa wateja ya uraisishaji wa shughuli zao za kibenki.

“Leo ni siku kubwa katika historia ya Faidika tukiwa tunazindua huduma mpya ya kifedha kutoka Faidika ambayo inaendana na lengo chapa la  taasisi yetu la “kuboresha maisha” ambayo ni njia yetu mpya kwa wateja katika kuwaraisishia shughuli zao za kibenki kupitia Executive Loan,” alisema Bw. Dlamini.

Bw. Dlamini alisema kuwa katika kipindi cha miaka kumi ya Faidika, ikitoa huduma mbali mbali za kifedha kwa watu wasiofikiwa zaidi na huduma hiyo katika imekuwa ndiyo chachu ya taasisi hiyo kufikia lengo lake la kujenga taasisi iongozayo katika ushawishi wa kutumia huduma za kibenki nchini.

“Tukizungumzia suala la ushawishi dhidi ya matumizi ya huduma za kifedha, kama tunavyo hapa Faidika ‘Inclusive Finance’, tunaelewa kuwa huduma za kifedha zinazidi kukua na ili kufikia lengo inatubidi kuendelea kukidhi mahitaji yanazozidi kuongezeka kwa wateja wetu kwa kuwapatia ya uraisishaji huduma kama hii ya Executive Loan ambayo imeundwa kipekee kikidhi matakwa yao.

Tunajivunia kwa kupata nafasi inayotustairi. Muhimu zaidi tumeweza kufanya hivyo tukiongozwa na misingi imara ya utoaji wa huduma ya fedha rahisi, inayofaa na nafuu kwa zaidi ya watanzania 45,000 nchi nzima.

Executive Loan ni suluhisho la kiushindani kwa soko la Tanzania, mkopo huo ukiwa hauna makusanyo ya ada au ada zilizojificha,” alisema.

Mkopo huo umeandaliwa ili kuitikia matakwa ya wateja kwa suluhisho ambalo limewalenga wateja ili kurahisisha shughuli zao za kifedha.

“Tunaamini katika thamani itakayongeza, ukiwa upatikanaji

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.