}

Guardiola ndiye kocha bora Duniani.

Pep Guardiola. 
Straika wazamani wa Bercelona Samuel Eto'o amemtaja meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuwa ndiye kocha bora Duniani.
Samuel Eto'o. 
Guardiola ameweza kushinda mechi 10 katila mechi zake kimi zakwanza akiwa na City lakini tangu awe chini ya uchunguzi amekuwa na matokeo yasiyoridhisha.
Man city ameenda mechi sita bila ya ushindi baada ya ushindi alioupata dhidi ya West Brom na Barcelona, lakini alitoka sare na Middlesbrough nakupigwa 3-1 na Chelsea katika uwanja wao wa Etihad siku ya Jumamosi, matokeo yaliyopelekea wawe nyuma kwa pointi 04 kwa kinara wa Ligi.

Eto'o alishinda mataji matatu chini ya Guardiola katika msimu wake wa kwanza Nou Camp.

Eto'o amesema Guardiola atabaki kuwa bora kwakuwa nguvu zake ni kubwa na huwa habadilishi mawazo yake,  na ememaliza kwakusisitiza kuwa kitaalamu Pep bado ni bora.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.