MFUNGAJI BORA NA MVP WA IVORY COAST ATUA YANGA SC
RASMI: Klabu ya Yanga imethibitisha kuinsa saini ya Kiungo Mshambuliaji hatari raia wa Ivory Coast Celestin Ecua kutoka klabu ya Zoman FC ya nchini kwao.
Mchezaji Ecua mwenye umri wa miaka 23 msimu uliopita akiwa na Zoman FC alifunga magoli 15 na kusaidia mingine 12 kwenye michuano yote huku alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP) wa ligi kuu nchini Ivory Coast na kufanya vizuri akiwa kwa mkopo Asec Mimosas katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Mbali na kuwa mchezaji bora wa ligi kuu Ivory Coast Celestin Ecua amefunga mabao 11 kwenye mechi 15 sawa na dakika 308' akifungana mbio za ufungaji na wachezaji kama Dramane Kamagate goli 11 wa klabu ya San Pedro aliyefunga magoli pia magoli 11 sawa na mchezaji wa timu ya Mouna d' Akoupe, Ako Isaac aliyefunga magoli 11 kwenye ligi kuu.
Usajili wa Celestin Ecua unakuwa usajili wa saba (7) mpaka sasa kwenye utambulisho wa kikosi cha Yanga SC baada ya usajili wa mshambuliaji Andy Boyeli (24) kutokea Sekhukhune ya Afrika Kusini ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa msimu (MVP) ligi ya Zambia akiwa na Power Dynamos sambamba na kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi ya Zambia akifunga mabao 18.
Mbali na sajili hizo,usajili mwingine wa Yanga sc mpaka sasa ni pamoja na beki Abubakar Nizar Othuman (Ninja), Kiungo Moussa Balla Conte, Winga Offen Chikola, Kiungo Abdulnasir Mohamed na kocha Romain Folz ambao wametambulishwa mpaka sasa kunako viunga vya Jangwani.
No comments