}

YANGA YASHUSHA MASHINE NYINGINE YAMPA NAMBA YA 8 KURITHI MIKOBA YA AUCHO


RASMI: Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Lassine Kouma kutokea klabu ya Stade Mallien ya nchini kwao.

Kouma mwenye umri wa miaka 21 raia wa Mali mwenye uwezo wa kucheza namba 10 uwanjani ametambulishwa kunako klabu hiyo ya Jangwani na kukabidhiwa jezi namba nane (8) ambayo ilikuwa inavaliwa Khalid Aucho ambaye tayari Yanga sc imeachana na mchezaji huyo.

Usajili wa Lassine Kouma unakuwa usajili wa nne (4) mpaka sasa kwenye kikosi cha Yanga SC baada ya Moussa Balla Conte, Offen Chikola na Abdulnasir Mohamed ambao wametambulishwa mpaka sasa kunako viunga vya Jangwani.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.