RAIS DKT SAMIA MGENI RASMI UFUNGUZI KITUO CHA EACLC
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalum ya kiuchumi Nchini Tanzania -TISEZA, Gilead Teri amesema kukamilika kwa kituo cha biashara na usafirishaji cha Afrika mashariki -EACLC, itasaidia kuongeza thamani yabiashara ya mauzo kwa zaidi ya bilioni 300 kwa mwaka.
Ametoa kauli hiyo katika kuelekea ufunguzi wa kituo hicho Agosti 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Amatumia nafasi hiyo pia kuzielekeza halmashauri nyingine kutenga maeneo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kama hiyo ili kuleta uchechemuzi wa uchumi na kuchangia ukuaji wa pato la Taifa kupitia kodi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Kituo cha biashara na usafirishaji cha Afrika Mashariki -EACLC, Cathy Wang amewataka wafanyabiashara Nchini kuchamkia fursa ya uwepo wa kituo hicho ili kujikwamua kiuchumi.
Utekelezaji wa kituo hicho umeanza mwezi Mei 2023 na umekamilika mwaka huu ambapo umegharimu shilingi bilioni 282.7 hadi kukamilika kwake na kinatarajiwa kuzalisha ajira rasmi zaidi ya elfu 15 na 5,000 zisizo rasmi.
No comments