}

WATUHUMIWA 17 WAPO MKONONI MWA POLISI KWA KOSA LA MAUAJI- MORCASE

JESHI la polisi mkoani Pwani, linawashikilia watuhumiwa 17 wakiwemo waliokuwa viongozi wa Serikali za mtaa kwa kosa la mauaji ya Sebastian Moshi (33) mkazi wa Ubungo, Kibangu jijini Dar es salaam yaliyotokea, kata ya Mapinga, wilayani Bagamoyo ,mkoani Pwani. 

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Salim Morcase ameeleza, tukio hilo limetokea julai 15 mwaka huu, huko maeneo ya Tungutungu, kata ya Mapinga, Bagamoyo Imani Mmasi, mkazi wa Sinza Dar es salaam alifika kwenye eneo lake lenye ukubwa wa hekari 10 akiwa na walinzi wake ili kufanya usafi na kuweka mipaka. 

Kutokana na tukio hilo, mtu mwingine Ismail Abbas Omary amepata majeraha makubwa ambapo anaendelea na matibabu hospital ya Rufaa ya Tumbi. 

Morcase ameeleza, chanzo cha tukio ni uvamizi holela wa ardhi na ametoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. 

Wakati huohuo katika tukio jingine la mauaji,jeshi hilo linamshikilia Rajabu Musa (23) mkazi wa mtaa wa Muheza,Kibaha kwa mauaji ya baba yake mzazi Hamis Said (50) . 

Morcase amefafanua , mtuhumiwa huyo alimshambulia baba yake mzazi, kwa kumpiga ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumtumbukiza kwenye shimo la choo.

 

Mwisho

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.