}

WATU 524 WAPIMA DNA KUJUA UHALALI WA WATOTO WAO- DKT.FIDELICE MAFUMIKO

Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan katika ununuzi wa mitambo na vifaa vya kisasa, umesaidia kuboresha huduma za uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara nchini.

Mafanikio hayo yametangazwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dokta Fidelice Mafumiko katika mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Uwekezaji huo umewezesha ongezeko la thamani ya mitambo ya shilingi Bilioni-17.8 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo kiasi hicho kimetumika kununua mitambo mikubwa 16 na midogo 274, iliyosaidia kuboresha ufanisi wa uchunguzi wa kimaabara kwa wananchi kuhusu sampuli za majanga.

Hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu, watu 524 wamepima DNA kwa ajili ya uchunguzi ili kujua uhalali wa watoto wao.
Aidha, Mkemia Mkuu amesema gharama ya kupima DNA ni shilingi laki moja kwa kila mtu, na matokeo ya uchunguzi huo hubaki kuwa siri ya mhusika.

Kuhusu udhibiti wa kemikali, Mamlaka inatekeleza jukumu kulingana na Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani namba 3 ya mwaka 2003 inayolenga kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya athari za kemikali.
Aidha, vibali vya kuingiza/kusafirisha Kemikali vimeongezeka kutoka 40,270 mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia zaidi ya Elfu-67 mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 40.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.