}

HATMA YA WAGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI CCM KUJULIKANA JULAI 28

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM,kimetaja sababu za kusogeza tarehe ya vikao vya uteuzi kuwa ni idadi kubwa ya  wagombea waliojitokeza kugombea nafasi za ubunge,uwakilishi na udiwani ndani ya CCM.

Kufuatia mabadiliko hayo Kikao ch Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM,kitakutana Julai 28,Mwaka huu kwa ajili ya uteuzi wa mwisho wa majina ya wagombea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma,Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo,CPA Amos Makalla amesema kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM,NEC kitakutana  Julai 26,Mwaka huu,kikifuatiwa na vikao vingine.

"Ndugu zangu niwaambie CCM inajivunia wagombea wake,na yeyote atakayesimama kugombea nafasi yoyote ni mtu aliyepimwa na anayetosha,niwaombe wagombea wawe watulivu wakati mchakato ukiendelea,"amesema.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.