}

AISHI MANULA AREJEA AZAM FC


Klabu ya Azam fc imethibitisha kumrejesha golikipa Aishi Manula kama mchezaji wao mpya klabuni hapo kwa mkataba wa miaka mitatu (3) utakaombakisha klabuni hapo mpaka mwaka 2028.

Manula mwenye umri wa miaka 29 golikipa wa kimataifa wa Tanzania (Tanzania One) anarejea tena Azam Fc baada ya kupita takribani miaka nane (8) tangu aondoke klabuni hapo mnamo mwaka 2017 akitimkia Simba sc alikodumu mpaka sasa.
Usajili wa Manula ndani ya Azam Fc  unafanya kuwa usajili wao wa nne (4) katika harakati za kujindaa na mashindano ya msimu 2025/2026 ikiwa tayari wamekamilisha usajili wa mlinzi wa kati Lameck Elias Lawi kutokea klabu ya Coastal Union, mshambuliaji Muhsini Malima kutokea Zed Fc ya nchini Misri pamoja na kocha mkuu Florent Ibenge kutokea Al Hilal Omdurman ya Sudan.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.