CGI. MAKAKALA ASHANGAZWA NA MIRADI YA MAGEREZA
Na. Stephan Ngolongolo - Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dk.Anna Makakala leo 22.9.2021,amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza zilizopo Msalato JIjini DODOMA kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi.
idha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dk.Anna Makakala amempongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleiman Mzee kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa na Jeshi Hilo.
"Mi nashangaa Kila sehemu ninayokwenda naona Mambo mengi,niwapongeze wewe na timu yako Mimi nakuja kidogo kidogo siwezi kukufikia wewe"Alisema CGI - Dk Makakala.
CGI Dk.Makakala alisema kwa Sasa Wana kiwanda cha ushonaji nguo ambacho kwa siku wanashona pea ishirini,pia amemwomba CGP wataalam kutoka Jeshi la Magereza waweze kufanya shughuli ambazo wameanza.
Awali CGP Suleiman Mzee alimweleza CGI Dk.Makakala jinsi alivyoweza kufanikisha miradi mbalimbali katika Jeshi,alimweleza kuwa alisimamisha shughuli binafsi zinazofanywa na Askari katika maeneo ya Jeshi Kama kilimo na mifugo kutokana na matumizi mabaya ya rasilimali zilizopo.
"Mimi sikufahamu Kama Magereza Kuna wasomi wa kufa mtu wapo na hawatumiki,na Mimi sikutafuta toka nje wataalam wowote huku Kuna Kila aina ya wasomi wapo wa Kila aina"alisema CGP Mzee.
Kwa upande wa maafisa waandamizi wa Magereza walimweleza CGI kuwa Jeshi la Magereza Lina hazina kubwa ya rasilimali mbalimbali na wataalam wenye weledi wa Hali ya juu wawatumie.
No comments