}

Tanzania na Kenya zajadili kujiimarisha kimahusiano.

Na. Anaseli Stanley Macha.


Tanzania na Kenya zinajadili mambo mbalimbali ikiwemo mahusianao na kutatua changamoto zilizopo ili kuimarisha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katibu mkuu wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki balozi Dkt. Aziz Mlima amesema mkutano huo wa siku tatu umeanza kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali ikiwemo makubaliano ya kielimu, kibiashara, ulinzi na afya.

Dkt. Mlima amesema Tanzania na Kenya zinaendelea kushirikiana katika masula ya utalii,usafiri wa anga,Afya, masuala ya kieleimu na hakuna mzozo kama inavyoelezwa ambapo serikali ya awamu ya tano inaendelea kuimarisha mahusiano na kufanya mikutano na nchi mbalimbali.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.