Simba wapata pigo, Wachezaji na makocha wakigeni wapigwa stop kucheza, Yanga wao shwari
Dar Es Salaam-Tanzania.
Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba hawataweza kuwatumia wachezaji wao wote wa kigeni katika mechi zijazo mpaka watakapopata vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.
Kwa mujibu wa habari kutoka Idara ya Uhamiaji, Simba imeajiri raia wa kigeni kumi ambao ni wachezaji saba na makocha watatu.
Idara ya Uhamiaji pamoja na TFF zimetoa tamko la kutotumika kwa Janvier Bokungu, Goue Noel Blagnon, Laudit Mavugo, Daniel Agyei, James Kotei, Method Mwanjale pamoja na benchi la ufundi, Joseph Omog, Jackson Mayanja na kipa wa makocha, Abdul Idd Salim.
Mchezaji mwingine wa kigeni, Juuko Murshid hayupo nchini hivyo hakuhusishwa katika zuio hili, Juuko yupo kwao katika kambi ya timu ya taifa ya Uganda inayojiandaa kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika.
Yanga Haina wasiwasi kwa hili.
Idara ya Uhamiaji nchini imetoa orodha inayothibitisha waajiriwa wote wa kigeni wa klabu ya Yanga kuishi na kufanya kazi nchini kihalali.
Kwa mujibu wa orodha hio ya Uhamiaji Yanga imeajiri wachezaji saba wa kigeni na makocha watatu wa kigeni na kukamilisha taratibu zote za uhamiaji, wizara ya Kazi, Ajira,Vijana na watu walemavu na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kupatiwa vibali vyao.
Orodha hio imetolewa na afisa wa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule na kuonesha wachezaji Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Vincent Bossou, Justine Zulu wamekatiwa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.
Pia makocha George Lwandamina na msaidizi wake Noel Mwandila pamoja na mkurugenzi wa ufundi, Hans Van Der Pluijm wana vibali vya kuishi na kufanya kazi.
No comments