}

Mjue mshindi wa mchezo wa Leo kati yaLiverpool na Everton kupitia Uchambuzi huu.


NaAnaseli Stanley Macha.




Everton na Liverpool wanajiandaa kuelekea katika mchezo wao wa ligi kuu ya England ambapo mchezo huo unapowakutanisha vigogo hao unakuwa na mtazamo mingi tofauti kutokana na uhasimu wa vilabu hivi ambavyo vyote vinatoka katika mji mmoja.

timu hizi zinapokutano mchezo huo huwa unaitwa  Merseyside derby  na leo hapo baadae tutashuhudia timu hizi zikikutana ambapo liverpool itasafiri hadi hapo Goodison Park kucheza na wenyeji wao Everton. 

Kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa liverpool Jurgen Klopp anaiongoza timu hiyo katika uwanja wa Goodison Park kuwakabili everton ambapo lengo lake katika msimu huu ni kuona anatwaa kikombe cha ligi hiyo ambapo itatokana kushinda katika michezo yake ya ugenini na hata ile ya nyumbani kwa asilimia kubwa ili kujihakikishia anakusanya alama nyingi zaidi. 

Lakini kikosi cha Everton ambacho kinaongozwa na kocha Ronald Koeman kina mtazamo wa kuendelea kulinda furaha yao ambayo imetokana na kupata ushindi wakitoka nyuma kwa jumla ya bao moja  katika mchezo wake dhidi ya Arsenal mchezo uliopigwa katikati ya wiki iliyopita .

Nafasi ya ushindi ikoje. 

Everton

kutokana na ushindi walioupata dhidi ya Arsenal inawapa nguvu kubwa ya kuwa na matokeo mazuri katika mchezo huu ambapo pia kucheza katika uwanja wa nyumbani kunakuwana faida ya kuwa na ushindi kutokana na uwepo wa mashabiki wengi pamoja na uzoefu wa uwanja weo.

Everton wanaweza wakatumia ubovu wa safu ya ulinzi  ya liverpool ili kuweza kupata matokeo ambayo yanaweza yakawashangaza wengi. 

Pia roho ya kupambana waliyoionesha katika mchezo wa dhidi ya Arsenal kama wataitumia tena katika mchezo wa leo pia itaweza kuwapa matokeo everton.

Ubora wa klabu ya everton chini ya kocha Ronald Koeman imeongezeka sana kwa sasa ukiangalia uwezo wa wachezaji kama Romelu Lukaku, Ross Barkley,Leighton Baines ambao wamekuwa na chachu kubwa ya kuwa na matokeo katika michezo yao kutokana  na mfumo ambao kocha huyo anautumia 
niseme tu katika mchezo huu Lukaku anaweza kuwa mwiba sana kwa livepool na ndie atakaeipatia bao la kwanza everton.

LIVERPOOL. 

Klabu ya liverpool Wanaweza kutengua msemo wa wahenga ambao unasema "mcheza kwao hutuzwa"  kutokana ligi ya uingereza ni ya tofauti  ambapo ushindi haujalishi ni wapi anacheza.

Uwezo wa kocha Jurgen Klopp na mfumo wake wa kutumia viungo wengi zaidi watakuwa na nafasi ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa ambapo moja ya njia ya kujilinda ni kumiliki vizuri mpira 
Ingawa historia za vilabu hivi zinapokutana katika uwanja huu zinalingana kwa kiasi kikubwa.

Liverpool ya sasa imeonekana kuimarika vizuri sana jambo ambalo leo linaweza kuleta matokeo kwa upande wao ambapo itategemea sana uwezo kiungo kinda raia wa ujerumani Emre Can na muingerza Jordan Henderson kupandisha timu katika eneo la hatari la everton ambapo kwa uwezo wa washambuliaji wa livepool wakiongozwa na Sadio Mane huenda wakaleta madhara makubwa kwa everton. 

Pamoja na ubovu walionao liverpool katika safu ya ulinzi  liver imemarika zaidi katika viungo na hata washambuliaji  ambapo katika msimu huu wa ligi kuu ya uingereza naweza kusema wako vizuri zaidi katika ushambuliaji. 

Klopp atakuwa na jukumu la kumuanzisha golikipa Simon Mignolet amabe mara nyingi anakuwa msaada mkubwa sana wakati timu hizi zinapo kutana kutokana na ubora wake wa kuweza kuficha na kupangua michomo ambayo inakuwa imeelezwa golini kwake.

Viwango na uelewanao wa  wachezaji Adam lalana Divock Orig Sadio Mane na Firmino hakika utaisumbua sana safu ya ulinzi ya everton katika mchezo wa leo.
Lalana na Mane leo kila mmoja atakuwa na hamu ya kuanza kuipatia bao na naona kila mmoja atapata bao kwa upande wao. 

mwisho 
EVERTON                      VS                      LIVERPOOL 
25%                         40%                          35%

HISTORIA. 
Hii ni mechi ya 227 katika michuano yote, na 195 ni michezo ya ligi , liverpool imefanikiwa kushinda michezo 74 everton 57 na kutoka sare 63 
Liverpool haijafungwa haijawahi kufungwa katika michezo 11 ya ligi walipokutana na  Everton  ambapo liverpool ilishinda michezo 4, na kutoka sare michezo 7 

Michezo minne iliyopita kwa timu hizi zilipokutana katika uwanja wa  Goodison Park hakuna timu iliyotoka na ushindi. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.