}

Chelsea yakubali kumuuza Oscar kwa klabu ya Shanghai SIPG kwa Euro milioni 60.

Oscar. 

Klabu ya Chelsea imekubali umuuza mchezaji Oscar kwa klabu ya shanghai SIPG kwa dau la £60milioni

Kiungo huyo raia wa brazil anatarajia kundoka hapo darajani katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili ambalo linafunguliwa kuanzia januari 12 mwakani  ambapo Oscar ataungana na mchezaji mwenzie ambae pia ametokea katika klabu hiyo ya Chelsea na timu ya taifa ya Brazil Ramires ambae alijiunga na klabu ya Jiangsu suning hivyo sasa watakuwa wakicheza ligi moja .

Klabu ya Chelsea kama itafanikiwa kumuuza mchezaji Huyo kwa dau hilo basi wataweka historia mpya ya kuuza mchezaji kwa gharama kubwa zaidi ambapo mpaka sasa inashikiliwa na usajili wa beki david luiz ambae alisajili kunako klabu ya PSG kwa dau la £50 milioni

Oscar alisajiliwa na klabu ya Chelsea tangu mwaka 2012 na amefanikiwa kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na kuweza kunyakuwa kikombe  cha ligi yaan premier league,  kile cha europa ligi na cha kombe la ligi ambapo yote ni katika kipindi cha miaka minne na nusu aliyokuwemo ndVillas-Boass katika kikosi hicho.

Uhamisho huu huenda ukamfanya Oscar kuwa chini ya kocha wake wa zamani wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.