}

ZAIDI YA SHILINGI BIL 86 ZAPATIKANA HARAMBEE YA CCM

Zaidi ya Shilingi Bilioni 86 zimepatikana katika Harambee ya Chama cha Mapinduzi iliyolenga kukusanya fedha kwa ajili ya Kampeni za chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Katika kiasi hicho Fedha Taslimu ni Shilingi Bilioni 56 na ahadi ni zaidi ya Shilingi Bilioni 30.

Akizungumza katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambako kulifanyika hafla hiyo, Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Samia Suluhu Hassan, amewashukuru wana CCM na makundi yote ambao wamechangia na watakaoendelea kuchangia ili kukiwezesha chama hicho kufanya Kampeni zake kwa ufanisi.

Rais Dokta Samia amesema chama kinajengwa na wanachama wake na ametumia muda huo kuhimiza mshikamano ndani ya CCM.

Awali Akitangaza matokeo ya michango hiyo Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dokta Emmanuel Nchimbi amesema zoezi la michango bado linaendelea.

Katika Harambee hiyo CCM ililenga kukusanya Shilingi Bilioni 100.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.