}

WATANZANIA WAHIMIZWA KUZINGATIA VIGEZO TUZO ZA NYERERE

MWENYEKITI wa Kamati ya Tuzo za Taifa za Mwalimu Nyerere Prof. Penina Mlama, amewasisitiza Watanzania wote wanaoshiriki katika uwasilishaji wa miswada kwa lengo la kushiriki kinyang'anyiro cha tuzo hizo kuzingati vigezo, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kuepuka kazi yake kuondolewa.

Akizungumza  Mkoani Dar es Salaa Prof. Penina alisema katika awamu tatu zilizopita walibaini changamoto ya watu kutofuata utaratibu na masharti yaliyoainishwa jambo linalosababisha kazi zao kuondolewa hata kama ni nzuri, akisisitiza kwamba katika msimu wa nne ambao dirisha linafungulia kesho miswada inakayopitishwa ni ile iliyozingatia vigezo pekee.

Akitolea mfano wa tatizo hilo amesema kuna watu wanawasilisha kazi nzuri lakini kigezo kinamtaka kwenye ushairi vigezo vinamtaka alete mashairi yasiyopungua 50 na yayosizidi 60 laki wanawasilisha 70, pia katika tamthilia alieleza kuwa hayatakiwi kuzidi maonyesho sita lakini wengine wanawasilisha nane, na kwamba hilo linasababisha kazi kukosa vigezo.
 
Aliongeza kuwa washiriki ni lazima wawe watanzania, kazi iwe mpya isichapishwe kokote, mwandishi ataruhusiwa kushiriki nyanja mojawapo kati ushairi, hadithi za watoto, riwaya na Tamthilia, andiko bunifu litakalowasilishwa liwe makini lililojikita katika masuala muhimu ya kijamii. 

Pia alisema katika tuzo hizo mshindi wa kwanza atapata Sh. Milioni 10, na kitabu chake kuchapishwa serikali itanunua nakala na kuzisambazwa katika shule zote nchini, wa pili atapata Sh. Milioni saba cheti, na wa tatu Sh. Milioni tano, akisema zawadi hizo ni kwa kila nyanja.

Hata hivyo, alieleza kuwa kutokana na umuhimu wa tuzo hizo kitaifa serikali imewekeza katika kuhakikisha wanafanikiwa kukuza kizazi kipya cha waandishi, kuchochea usomaji na soko la vitabu, kukuza Kiswahili, kuchochea ujifunzaji na kuongeza idadi ya vitabu nchini.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dk. Aneth Komba, alisema lengo mojawapo la tuzo hizo lilikuwa ni kuongeza idadi ya machapisho akisema: "Kama taasisi ambayo inasimamia upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na ujifunzaji, tulikuwa tunaona kuna changamoto ya vitabu vya hadithi ambavyo vimeandikwa na wazawa, na faida tuliyoipata baada ya ujio wa tuzo, tunajivunia kuongezeka kwa maandiko yanayoakisi mila na tamaduni zetu".

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.