UDP WAAHIDI KUTETEA WANYONGE
Mgombea Urais kupitia Chama cha United Republic Party (UDP),Saum Hussein Rashid, ameanza safari ya kuwania nafasi ya Urais huku akiahidi kuleta maisha bora kwa watanzania kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa kawaida.
Mgombea huyo amefika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma, Agosti 15, 2025,akiwa ameambatana na mgombea mwenza wake Juma Khamiss Faki na kupokelewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu, Saum ameeleza kuwa kipaumbele chake ni kuinua hali za wananchi wanyonge kwa kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu kama maji safi na salama, elimu bora, huduma za afya, pamoja na kukuza sekta ya viwanda na biashara.
Aidha, amesisitiza kuwa UDP itaendelea kudumisha misingi ya amani na utulivu ambayo imekuwa nguzo muhimu ya Taifa kwa miaka mingi, na kwamba chama hicho kitaelekeza viongozi na wanachama wake kuendesha kampeni kwa njia ya kistaarabu, kuheshimu sheria na kutumia njia sahihi za utatuzi wa changamoto zozote zitakazojitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi
No comments