}

JONATHAN SOWAH AJIUNGA NA SIMBA SC

RASMI: Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji Jonathan Sowah kuwa mchezaji wao mpya kwa mkataba wa miaka miwili (2) utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2027 akitokea Klabu ya Singida Black Stars.

Sowah mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ghana akiwa na Klabu ya Singida Black Stars msimu uliomalizika 2024/2025 alifunga mabao 13 kwenye michezo 15 ya ligi kuu.

Usajili na Jonathan Sowah kwa wekundu wa msimbazi Simba sc unakuwa usajili wa tano (5) klabuni hapo baada ya usajili wa beki Rushine De Reuck, Kiungo Alassane Maodo Kante, Winga Morice Abraham, Kiungo Mkabaji Hussein Daudi Semfuko kutokea klabu ya Coastal Union.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.