}

BRELA NA BASATA KUSHIRIKIANA KUSAJILI ALAMA ZA BIASHARA

Wakala wa usajili wa Biashara na leseni -BRELA kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa -BASATA imeingia mashirikiano yatakayojielekeza katika kubadilishana taarifa kupitia TEHAMA pamoja na kuwezesha usajili wa alama za biashara.

Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati wa kusaini makubaliano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu -BRELA, Godfrey Nyaisa amesema ushirikiano huo ni sehemu ya kuchochea maendeleo ya sekta ya ubunifu na sanaa Nchini.

Amesema maeneo mengine ni kutambua uhalali wa biashara, usajili wa miliki ubunifu na utambuzi wa mchango wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa -BASATA, Dkt Kedmon Mapana ameiekeleza -BRELA kuwekeza zaidi katika utoaji wa Elimu kwa wasanii kuhusu umuhimu wa kusajili alama za biashara zao.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.