WADAU WA MAZINGIRA (JET ) WAKO TAYARI KUTEKELEZA DIRA YA MAENDELEO 2050
WADAU wa Mazingira Nchini wamesema wako tayari kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 katika kuhimiza uchumi wa buluu ambapo ndani ya miaka mitatu katika eneo la Tanga na Pemba zaidi ya hekta 90 za mikoko zimerejeshwa kuimarisha uthabiti wa fukwe na kuboresha uchumi wa wananchi wa maeneo hayo.
Wadau hao ni Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania(JET) kwa kushirikiana na Taasisi ya kimataifa ya Masuala ya Hifadhi na Mazingira(IUCN) kupitia miradi ya Bahari Mali na kuwa stari wa mbele kuwahamasisha wananchi kufanya shughuli endelevu na rafiki lwa mazingira.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi pana zinazoongozwa na jamii katika uhifadhi wa mazingira ya baharini katika eneo la Tanga–Pemba, ambazo tayari zimeleta manufaa makubwa ya kiikolojia na kiuchumi
Akizungumza na katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya uchumi wa buluu, yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania(JET) na Taasisi ya kimataifa ya Masuala ya Hifadhi na Mazingira(IUCN) kupitia mradi ya Bahari Mali, Meneja wa Miradi ya Uhifadhi wa Bahari Joseph Olila alisema urejeshwaji huo ni sehemu ya mradi wa Bahari Mali unaolenga kutumia fursa ya uchumi wa buluu kwa njia jumuishi na endelevu kwa lengo la kulinda bayoanuwai ya Pwani na baharini.
Pia, mradi huo unahusisha upandaji wa mikoko katika maeneo yaliyoharibiwa na kuwajengea uwezo wanajamii katika shughuli mbadala za kiuchumi kama vile ufugaji wa nyuki sio kusaidia malengo ya mazingira tu bali na kuongeza kipato kwa kaya husika.
Akizungumzia mradi huo alisema lengo ni kusaidia shughuli za uchumi wa buluu katika eneo la Tanga kwa wilaya ya Mkinga, Pangani na Pemba kwa wilaya mbili ambazo Mkoani na Micheweni.
Alisema program hiyo imewawezesha wananchi kujikwamua na umaskini na kufanya shughuli zao ambazo ni endelevu na rafiki kwa mazingira.
Kuhusiana na tafiti kwa kushirikiana na wadau wengine wamefanikiwa kuangalia eneo la asidi katika bahari hivyo mradi huo utawasaidia wanajamii kutambua fursa zitokanazo na bahari na kurejesha uoto wa asili.
Kwa upande wake, Mtafiti Mwandamizi Asasi ya Utafiti Uvuvi Tanzania (TAFIRI),Rushingisha George alisema wakiwa wanafanya tafiti wanatarajia matokeo ambayo yatumike kuboresha shughuli zote za uhifadhi.
No comments