}

SIMBA SC NA USAJILI MPYA, MDHAMINI MPYA NA JEZI MPYA

RASMI: Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati Rushine De Reuck kutokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini kwao kwa mkataba wa mwaka mmoja (1) wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 raia wa Afrika Kusini mwenye uwezo wa kucheza mlinzi wa kati,mlinzi wa pembeni na kiungo mkabaji anaenda kuchukua nafasi ya Che Fondoh Malone aliyetimkia klabu ya USM Alger ya nchini Algeria. 

Usajili wa Rushine De Reuck unakuwa usajili wa kwanza kunako kikosi cha Simba sc baada ya tu kutamtangaza mdhamini mkuu mpya kampuni ya ubashiri ya Betway Tanzania ambayo siku ya leo imetoa jumla ya Tsh Bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu (3) klabuni hapo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.