}

MFUMO WA M-MAMA UMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO-DKT.MAGEMBE

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema mfumo wa usafiri wa dharura kwa mama mjamzito, aliyejifungua na mtoto mchanga(M-mama) umekuwa na mchango mkubwa katika kuokoa maisha.

Dkt. Magembe amesema hayo leo Julai 11, 2025  Jijini Dodoma wakati akitoa wasilisho kwenye Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaoratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

"Huduma ya M-mama imeendelea kuimarika siku hadi siku hasa katika kuokoa maisha ya mama na mtoto, hivyo imezaa matunda makubwa katika kuimarisha afya ngazi ya msingi," amesema.

Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri mwaka 2025 umeanza  Julai 11 hadi 13, 2025  na unatarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 12, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  huku ukienda sambamba na kaulimbiu isemayo”Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.