}

MAKALLA ASEMA UHALALI WA BARUA YA KUJIUZULU AULIZWE POLEPOLE

KATIBU wa Nec,Itikadi,Uenezi na Mafunzo,wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Amos Makalla,amesema barua ya kujiuzulu kwa Balozi wa Cuba Humphrey Polepole iliyosambaa mtandaoni ameisoma mtandaoni kama walivyosoma watu wengine hivyo uhalali wa barua hiyo wa kuulizwa ni Polepole mwenyewe.

Makalla ametoa kauli hiyo leo Julai 13,2025, Jijini Dodoma,wakati akijibu swali la waandishi wa habari katika mkutano wake kuhusu kuanza kwa vikao vya CCM ngazi ya Taifa.


“Nakiri kuisoma barua ya Polepole kama ambavyo na nyinyi mmeisoma,mwenyek uthibitisha kwamba barua halali ama sio halali ni yeye mwenyewe lakini mimi na nyinyi tumeisoma katika mtandao na maudhui yake nimeyasoma,sasa naamini kwamba mtapata nafasi ya kujiridhisha kwamba barua ile ni ya kweli,na akisema ni ya kweli basi amethibitisha barua ni yak wake,

“Kitu kikubwa nilichofurahi amemalizia kwak usema atabaki kuwa mwanachama mwadilifu wa CCM,kwa hiyo huyu bado ni mwanchama wa CCM,kama ni kweli tunamshukuru kwa maoni yake aliyoyatoa,na kama barua ni ya kweli basi ni mawazo yake,ridhaa yake,uamuzi wake,sisi tunaendelea na mchakato wa viongozi wetu kwa ajili ya uchaguzi wa Rais,Ubunge na Udiwani,”.amesema.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.