}

HIMID MAO (NINJA) ASAJILIWA AZAM FC

Rasmi klabu ya Azam Fc imethibitisha kumrejesha kumtambulisha kiungo Himid Mao Mkami kutokea klabu ya Ghazi El Mahalla ya nchini Misri kwa mkataba wa mwaka mmoja (1) mpaka mwaka 2026.

Himid Mao mwenye umri wa miaka 32 mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliwahi kuitumikia Azam Fc kuanzia timu ya vijana toka mwaka 2007 hadi mwaka 2018 alipoondoka nchini na kwenda kucheza soka la nje kwenye klabu ya Petrojet ya Misri.

Pia Himid Mao Mkami amecheza klabu ya ENPPI ambayo nayo ni nchini Misri kabla ya kujiunga na Ghazi El Mahalla ambayo ndio alikotokea huko na kujiunga na wanalambalamba Azam Fc kwaajili ya msimu ujao.

Usajili wa Himid Mao ndani ya Azam fc unakuwa ni Usajili wa nne (4) kwenye klabu hiyo baada ya Lameck Lawi, Muhsini Malima Aishi Manula na kocha Florent Ibenge.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.