CAF WATIA TIKI MAANFALIZI YA CHAN2024 TANZANIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limeridhishwa na maandalizi ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yanayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CAF, Veron Mosengo-Omba, leo Julai 22, 2025 baada ya kufanya ziara ya kukagua maandalizi hayo, ambapo ametembelea viwanja mbalimbali vya mazoezi pamoja na Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Uwanja wa Benjamin Mkapa umetangazwa kuwa wenyeji wa mechi ya ufunguzi ya mashindano hayo, ambapo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itapambana na Burkina Faso ambapo, CAF imeeleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa na maandalizi yanayoendelea.
"Tanzania iko kwenye mwelekeo mzuri wa kuandaa mashindano yenye viwango vya juu, "amesema Mosengo-Omba.
No comments