}

BALOZI MAPURI ATOA WITO WA UZINGATIAJI WA SHERIA UCHAGUZI

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri,  amesisitiza umuhimu wa kufuatwa kwa hatua na taratibu mbalimbali za kikatiba na kisheria ili kuondoa malalamiko au vurugu zinazoweza kutokea katika mchakato wa uchaguzi.

Balozi Mapuri ameyasema hayo leo Julai 21, 2025, mkoani Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Mafunzo hayo ambayo yanahusisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo, maafisa wa uchaguzi pamoja na maafisa wa ununuzi yanatarajiwa kuendelea hadi Julai 23, 2025. mafunzo kama hayo yanafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Rukwa, Mbeya, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.