}
­

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA RASMI TUZO ZA SERENGETI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua rasmi  tuzo za uhifadhi na utalii na kusisitiza kuwa Serikali itendelea kubuni mikakati ya kuimarisha sekta ya Maliasili na Utalii kwa kuwa sekta hiyo ni nguzo muhimu ya uchumi wa Taifa. 

Amesema hayo Desemba 20, 2024 alipozindua Tuzo za Serengeti katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. 

Lengo la Tuzo hizo ni kuchochea ushindani kati ya wadau wa sekta ya maliasili na utalii nchini. 

Amesema kuwa Sekta ya maliasili na utalii ni chanzo kikubwa cha mapato ya taifa kwa kuwa inahusisha shughuli nyingi za kiuchumi. 

Aidha, amefafanua kuwa Sekta hiyo inachangia asilimia 30.9 ya mapato ya fedha za kigeni ambapo asilimia 25 yanatokana na utalii, asilimia 5.9misitu na nyuki. 

Katika hatua nyingine, Waziri  mkuu Majaliwa amesema  juhudi za dhati na maono makubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa kwa asilimia 96 kutoka watalii 922,692 mwaka 2021 hadi watalii 1,808,205 mwaka 2023;


Waziri  mkuu Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaweka vigezo vya wazi na vinavyojulikana vya uteuzi na upokeaji wa tuzo. 

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dokta Pindi Chana amempongeza Rais Samia kwa namna anavyojitoa katika kuhakikisha Sekta ya Maliasili na Utalii inaendelea kukua kwa kasi. 

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuimarisha uhifadhi na kuendeleza utalii ikiwemo kutumia teknolojia mbalimbali pamoja kuendeleza Programu ya Tanzania – the Royal Tour na  kuibua mazao mapya ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.