}
­

CGP MZEE ATOA MAAGIZO UPANDAJI WA MITI KWA MAGEREZA NCHI NZIMA

 Na.Geofrey Jacka/Mfaume Ally - Kongwa.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Zahanati ya Gereza Kongwa.


KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, leo Februari 16,2022 ametoa Maagizo kwa Wakuu wa Magereza Mikoa, na Wakuu wa Gereza Nchi nzima, kuhakikisha Magereza yote yana anzisha Upandaji wa miti, ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango  alilolitoa hivi Karibuni.

Agizo hilo amelitoa Leo alipotembelea Gereza Wilaya Kongwa jijini Dodoma, kwaajili ya kuweka jiwe la Msingi katika nyumba za Maafisa na Askari zinazoendelea kujengwa, na kuzindua Zahanati ya Gereza hilo ambapo awali alipanda Miti miwili kama ishara ya uzinduzi wa zoezi la Upandaji wa miti ndani ya Jeshi la Magereza.

"Nawaagiza Wakuu wa Magereza Mikoa yote, kuanza zoezi la Upandaji miti, Kuna baadhi walishaanza, lakini kwa kupanda kwangu leo miti miwili hapa Kongwa ndio kuwe mwanzo rasmi wa Upandaji wa miti Nchi nzima ndani ya Jeshi la Magereza, na hili ni agizo pia alilolitoa Mh. Makamu wa Rais, hivyo  naagiza katika taarifa ile ninayoipokea kila siku ya Mifugo, kiongezwa na kipengele Cha taarifa ya miti, kila Gereze liniambie tumepanda miti Mitano, Kumi au Ishirini, na nitakuwa nafuatilia" aliongeza CGP. Mzee.

Aidha katika hatua nyingine amempongeza Mkuu wa Gereza Wilaya Kongwa SP. Tekla Ngilangwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na kujitegemea, kwani licha ya kuanzisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo, ameweza kufanya ukarabati mkubwa wa Gereza ambao hauwahi kufanyika tangu kuanzishwa kwa Gereza hilo mwaka 1949.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza Wilaya Kongwa SP.Tekla Ngilangwa, amemshukuru Kamishna Jenerali Mzee kwa kumuwezesha katika kuanzisha Miradi mbalimbali ukiwemo wa Tofali ambao imekuwa tegemeo Wilayani Kongwa.

ACP. Keneth Mwambije, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa Zahanati ya Gereza Kongwa, Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dr. Thomson Samwel, amempongeza Mkuu wa Gereza kwa kupokea na kuufanyia kazinushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya Afya wanayokuwa wana mshauri, huku akisema kuanzishwa kwa Zahanati hiyo kutasaidia Wananchi wa Kongwa hivyo amemuhimiza mkuu huyo wa Gereza kumaliza kwa haraka ujenzi wa Jengo la mama na mtoto.

Dr. Thomson Samwel, Mganga mkuu wa Wilaya ya Kongwa.

Miradi iliyotembelewa Leo ni pamoja na Nyumba tatu za makazi ya Maafisa na Askari ambazo CGP. Mzee ameziwekea Jiwe la Msingi, ambapo mpaka kukamilika kwake zitagharimu kiasi cha Shillingi Milioni 168, pia Amezindua kuanza kutumika Gari Isuzu (Tipa) ambalo limefanyiwa Matengenezo makubwa, pamoja na Uzinduzi wa Zahanati ya Gereza hilo.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.