Mtibwa Sugar yaipa Onyo Singida United.
![]() |
Kikosi cha Mtibwa Sugar kutokea Manungu Turiani mkoani Morogoro. |
Uongozi wa klabu ya mtibwa sugar umesema kikosi chao leo kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Manungu Turiani kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ambao watawakaribisha wakulima alizet wa singida Singida United.
Thobias Kifaru Ligalambwike Afisa habari wa klabu ya Mtibwa amesema pamoja na kuwa hawaja poteza mchezo wowote mpaka sasa wanaelekeza nguvu zao zote katika kuhakikisha wanaichakaza Singida katika uwanja wao wa nyumbani Hapo manungu siku ya jumapili.
kifaru amesema kikosi kina hali nzuri na wachezaji wana morali kubwa ya kupamba ili kuendeleza kasi waliyo nayo katika kuhakikisha kila mchezo msimu huu wanapata ushindi.
Pomoja na kwamba usaliji uliofanywa na kikosi cha singida united wa kucmchukua kocha bora Van Der Plujm wao hwana hofu ya kuwafanya washindwe kupata matokeo siku hiyo.
Kikosi cha mtibwa kinachonolewa na kocha Zuberi Katwira katika msimu huu kimefanikiwa kukusanya alama 15 wakiwa sawa na wekundu wa msimbazi simba na Yanga ambao wao hapo kesho watakuwa wakikipiga katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
No comments